Katika mkutano huo uliofanyika mjini Tehran mawaziri hao wawili wamejadili njia za kuimarisha uhusiano. Aidha Wizara ya Utamaduni na Elimu ya Cyprus imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Elimu ya Iran.
Cyprus ni nchi iliyo mashariki mwa Bahari ya Mediterranean kusini mwa Uturuki na magharibi mwa Syria na Lebanon.
Cyprus ni mwanachama mwanzilishi wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote na ilijiunga na Umoja wa Ulaya Mei Mosi 2004. Takribani asilimia 78 ya wakaazi wa nchi hiyo ni Wakristo na asilimia 18 ni Waislamu.
689592