Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Wanachuo Waislamu wa Marekani na Canada (Msanational), mashindano hayo yameandaliwa na jumuiya hiyo kwa lengo la kuwahimiza wanachuo Waislamu kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yatakuwa katika viwango viwili vya kuhifadhi Surat al Hujurat na Surat Yusuf.
Jumuiya ya Wanachuo Waislamu Marekani na Canada imeandaa darsa za kuhifadhi Qur'ani ili kuwatayarisha wanachuo wanaokusudia kushiriki katika mashidano hayo.
Jumuiya ya Wanachuo Waislamu wa Marekani na Canada ilianzishwa mwaka 1963 katika Chuo Kikuu cha Illinois cha Marekani kwa lengo la kuarifisha Uislamu na Waislamu na vilevile kukidhi mahitaji ya wanachuo Waislamu.
689728