IQNA

OIC yaonya kuhusu kuongezeka kwa visa vya chuki dhidi ya Uislamu

12:50 - November 07, 2010
Habari ID: 2026749
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imeonya kuhusu kuongezeka kwa visa vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu hususan wahamiaji katika bara la Ulaya.
Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu amesema, chuki hizo dhidi ya Uislamu zinashabihiana na zile za mwanzoni mwa karne iliyopita, wakati wa kuzaliwa, kukuwa na kusambaa kwa kasi sera za kifashisti na za kinazi.
Ihsanoglu amesema, badala ya mamlaka na vyama vya kisiasa ulimwenguni kupiga vita chuki dhidi ya Uislamu (Islamaphobia), vinatumia chuki hizo kujiongezea umaarufu na kupata wafuasi zaidi ili kujikuza na kupanua ushawishi wao katika uga wa siasa.
Katibu Mkuu wa OIC amelitaka bara la Ulaya kufumbua macho kuhusiana na kuhusu Uislamu na kuwacha kueneza kasumba potofu dhidi ya ulimwengu wa dini hiyo tukufu.
689581



captcha