Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu barani Ulaya Sufian Thauri amesema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa na wawakilishi na viongozi wa dini mbalimbali na kujadili maudhui ya mazungumzo kati ya dini tofauti.
Thauri amesema kuwa kwa sasa wanachuo 140 wa kike na kiume wanapata elimu katika chuo hicho. Thauri ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu Abdullah bin Abdul Muhsin al Turki.
al Turki amekaribisha suala hilo na kusema jumuiya yake iko tayari kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kiislamu barani Ulaya katika nyanja mbalimbali za kielimu, utamaduni wa Kiislamu, kuimarisha mazungumzo na kadhalika. 690167