IQNA

Jarida la Kiutamaduni la Iran lachapishwa kwa Kiingereza

12:24 - November 08, 2010
Habari ID: 2027702
Jarida la Kielektroniki la Kitengo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London limechapishwa chini ya anwani ya ICN-Iranian Cultural Newsletter.
Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu, toleo la kwanza la jarida hilo limetolewa Novemba 5. Kati ya maudhui ya toleo hilo ni hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu kuzingirwa pango la ujasusi (ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Tehran), hotuba za Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran kuhusu masuala mbalimbali ya Kisiasa, habari kuhusu mikutano ya mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London, n.k.
Jarida hili la kielektroniki litakuwa likitolewa mara moja kwa wiki na kuangazia masuala ya kiutamaduni, kisiasa na kijamii. Lengo la kuchapishwa jarida hilo limetajwa kuwa ni kusambaza kwa njia sahihi fikra na mitazamao ya viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran miongoni mwa wasomi na vyombo vya habari nchini Uingereza.
691018
captcha