IQNA

Hamas yalaani hatua ya Wazayuni kuharibu msikiti

16:12 - November 08, 2010
Habari ID: 2027847
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali vikosi vya utawala wa Kizayuni vilivyovamia na kuharibu msikiti wa mji wa Rahat.
Taarifa ya Hamas imesema, 'Wananchi Waislamu wa Palestina wanapaswa kuungana na kujiepusha na mifarakano ili wakabiliane ipasavyo na hujuma za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni'.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Hamas imetoa wito kwa nchi za Kiislamu, Waislamu kote duniani na jumuiya za kimataifa kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe hujuma na uharibifu wake dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu huko Palestina.
Jumamosi iliyopita, wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel waliushambulia na kuuharibu msikiti katika jangwa ya Neqab mjini Rahat.
Katika miezi ya hivi karibuni vikosi vya utawala wa Kizayuni vimeshambulia na kuvunjia heshima misikiti kadhaa ya Wapalestina mbali na kupanga njama za kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa. 690957
captcha