IQNA

Saudia yatangaza 16 Novemba kuwa sikukuu ya Idul Adh'ha

16:14 - November 08, 2010
Habari ID: 2027852
Saudi Arabia imetangaza kuwa tarehe 7 Novemba ni siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul Hijja na kwa utaratibu huo sikukuu ya Idul Adh'ha itakuwa tarehe 16 Novemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la The Peninsula' mahujaji watasimama Arafa tarehe 15 Novemba na siku itakayofuata watafanya amali za Idul Adh'ha.
Wakuu wa Saudi Arabia wametangaza kuwa kuwa mahujaji milioni mbili watashiriki katika ibada ya hija ya mwaka huu.
690582
captcha