IQNA

Waislamu wa Kenya waelekea Makka

16:38 - November 08, 2010
Habari ID: 2028003
Waislamu wa Kenya Jumamosi iliyopita walianza kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutekelesa ibada ya hija.
Shirika la habari la KBS limeripoti kuwa karibu Wakenya 300 waliondoka Mombasa alasiri ya Jumamosi iliyopita wakielekea Makka ambako watajiunga na Waislamu wenzao kutoka maeneo mbalimbali duniani na watakuwa huko kwa kipindi cha wiki mbili wakitekeleza ibada ya hija.
Benki ya First Community ndiyo iliyodhamini hija ya Waislamu wa Mombasa na imeahidi kufanya jitihada za kupeleka idadi kubwa zaidi ya Waislamu huko Makka bila ya kujali hali zao za kifedha.
Jamaa na marafiki wa mahujaji hao walimiminika katika uwanja wa ndege wa Moi kuwasindikiza na kuwaaga mahujaji hao.
Waislamu wengi wa Kenya wanaishi maeneo ya Pwani mwa nchi hiyo. 691315
captcha