IQNA

Kikao cha 'Uhuru wa Dini, Daraja la Uhusiano Baina ya Uturuki na Ulaya' kufanyika Brussels

18:11 - November 08, 2010
Habari ID: 2028049
Kikao cha Uhuru wa Dini, Daraja la Uhusiano Baina ya Uturuki na Ulaya kimepangwa kufanyika tarehe 16 na 17 Novemba katika makao ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji.
Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuchunguza hali ya dini zenye wafuasi wachache nchini Uturuki na kujaribu kuboresha hali yao na vilevile kustawisha uhusiano baina ya wafuasi wa dini mbalimbali nchini humo.
Miongoni mwa shakhsia watakaohudhuria kikao hicho ni kiongozi wa Jumuiya ya Alawiyyun ya Uturuki Metin Tarhan, Afisa wa Kanisa la Waarmeni wa Uturuki Aram Ateşyan na kiongozi wa Muungano wa Kimataifa wa Wakristo wa Kiasiriani Johny Messo.
Siku ya kwanza ya kikao hicho itajadili matatizo ya wafuasi wa dini za waliowachache nchini Uturuki na kikao cha siku ya pili kitachunguza njia za kustawisha uhusiano kati ya dini mbalimbali. 691095


captcha