IQNA

Wanachuo laki mbili kushiriki Mashindano ya Qur'ani katika Chuo Kikuu cha Azad

10:56 - November 09, 2010
Habari ID: 2028195
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad nchini Iran kimeandaa mashindano ya Qur'ani Tukufu yatakayowashirikishi wanachuo na wahadhiri zaidi ya laki mbili.
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Qur'ani katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad Abdulmajid Talebtash amesema usajili wa washiriki katika mashindano hayo ulianza Oktoba 2 na kumalizika Novemba 6. Hata hivyo kutokana na maombi ya wanachuo, muhula wa kujisajilisha umeongezwa.
Amesema mashindano hayo yatafanyika katika awamu tatu za mchujo, kieneo na kitaifa ambapo mashindano ya kitaifa yanatazamiwa kufanyika Mei 2011. Mashindano hayo yatakuwa katika viwango vya hifdhi, kiraa na vilevile adhana, tafsiri ya Qur'ani na Nahjul Balagha, sira ya Mtume SAW, fatwa za kidini na kuhifadhi ziara ya siku ya Ashura na Jamia Kabira.
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad kina matawi kote nchini Iran na hivi sasa kinakadiriwa kuwa na wanachuo Milioni 1.3. Chuo hicho kimetajwa kuwa cha tatu kwa ukubwa duniani. 690052
captcha