Taarifa iliyotolewa na Baraza la Kiislamu la Uingereza imesema kuwa kikao hicho kitachunguza mustakbali wa sekta na biashara ya nyama halali nchini humo na barani Ulaya na matatizo na changamoto zinazowakabili wazalishaji nyama halali.
Kikao hicho kitajadili masuala mbalimba kama suala la kustawishwa viwanda na biashara ya nyama halali, kushughulikia masuala ya watumiaji katika nchi za Magharibi, bidhaa za halali mahotelini na suala la kuanzishwa jumuiya rasmi za bidhaa halali katika nchi za Uingereza na Norway.
Kikao hicho kitasimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Halali (IHI) ikishirikiana na Idara ya Viwanda na Biashara ya Kiislamu ya Malaysia (ICCI) na wazalishaji wa bidhaa za halali. 692096