IQNA

Mkutano wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu kuanza kesho Makka

14:15 - November 10, 2010
Habari ID: 2029513
Mkutano wa 11 wa kimataifa wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu (MWL) utaanza kesho katika mji mtakatifu wa Makka. Mkutano huo utachunguza changamoto za vyombo vya habari katika zama za utandawazi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu (MWL) Abdullah bin Abdul Muhsin al Turki amesema kuwa mkutano huo wa kimataifa utahudhuriwa na maulamaa, wahubiri wa ulimwengu wa Kiislamu na viongozi wa vituo vya Kiislamu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Amesema kuwa maudhui zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na 'vyombo vya habari katika zama za utandawazi', 'familia na jamii na changamoto za vyombo vya habari', 'umma wa Kiislamu na changamoto za vyombo vya habari' na 'hatua za kielimu za kukabiliana na changamoto hizo'.
Maudhui nyingine zitakazojadiliwa ni 'maadili ya vyombo vya habari katika zama za utandawazi', 'sura ya Uislamu na Waislamu katika vyombo vya habari vya kimataifa', 'Waislamu na teknolojia ya habari', 'jamii na hujuma za kiutamaduni', 'vyombo vya habari vya Kiislamu, kanuni na sheria', 'vyombo vya habari na mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na kadhalika.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake Katibu Mkuu wa jumuiya ya MWL amesema kuwa msimu wa hija unatoa taswira kubwa ya umoja wa Waislamu na amevitaka vyombo vya habari ya ulimwengu wa Kiislamu kusisitiza juu ya masuala ya kimsingi kama umoja na mshikamano wa Waislamu na kadhia ya kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu. 692621



captcha