IQNA

Senegal kuingia Soko la Kifedha la Kiislamu

18:59 - November 10, 2010
Habari ID: 2029665
Senegal imesema itachapisha Hati za Dhamana za Kiislamu au Sukuk mwaka 2011 na hivyo kuwa nchi ya hivi karibuni ya Afrika inayojiunga katika Soko la Fedha la Kiislamu duniani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ibrahim Seck Mkuu wa Shirika la Kimataifa la SYM linalotoa huduma kwa wawekezaji wa kimataifa wanaotaka kuwekeza Senegal amesema, 'Waislamu ni asilimia 94 ya wakaazi wa Senegal kwa hivyo Benki za Kiislamu zinaweza kupata nguvu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi'. Seck ameongeza kuwa Senegal ina utulivu ikilinganishwa na nchi zingine za Kiafrika na hivyo inaweza kuwa kivutio kwa wawekezaji kutoka Ghuba ya Uajemi.
Duru zinaarifu kuwa Senegal inakusudia kutumia sukuk kuimarisha uhusiano na nchi za Mashariki ya Kati.
Weledi wa mambo ya kifedha wanasema kuwa asilimia sitini ya sekta ya kifedha ya Kiislamu duniani inayokadiriwa kuwa $ trilioni moja iko katika Ghuba ya Uajemi.
692431
captcha