Kwa mujibu wa tovuti ya hajinformation kongamano hilo linafanyika kwa himaya ya Wizara ya Hija ya Saudi Arabia kwa lengo kuongeza maarifa na kubadilishana mawazo kuhusu mitazamo mbalimbali ya hija na masuala husika. Aidha kongamano hilo linakusudia kutathmini njia za kuwahudumia mahujaji ili kuwawezesha watekeleze amali za hija kwa njia sahali bila matatizo.
Kongamano hilo la kimataifa limefunguliwa na Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Fuad bin Abdulsalam al Farisi na kuhudhuriwa na maulamaa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
692823