Wakibainisha suala hilo, viongozi wa serikali ya Paris wamesema kuwa tokea miezi mitatu iliyopita, wizara tatu husika za nchi hiyo zimekuwa zikiandaa na kufuatilia mambo yanayohitajika kwa ajili ya mahujaji na kwamba mazungumzo yamekuwa yakifanyika kati ya wizara hizo na Baraza la Waislamu la Ufaransa CFCM, ubalozi wa Saudi Arabia na mashirika ya huduma za safari za hija ili kuwahudumia kwa njia inayofaa mahujaji wa Ufaransa walio na nia ya kuhiji mwaka huu.
Serikali ya Ufaransa pia imechapisha vijitabu 42,000 vya maelezo mbalimbali kuhusu hija kwa ajili ya kutawanywa miongoni mwa mahujaji wa Ufaransa na kwamba imeanzisha ofisi itakayokuwa ikishughulikia masuala yao katika kipindi chote cha hija katika mji mtakatifu wa Makka. 692965