IQNA

Shughuli za Qurani kwa ajili ya familia Iran

13:05 - November 11, 2010
Habari ID: 2029940
Kituo cha Qurani cha Iran (Darul Quran) kinapanga shughuli kadhaa za Qurani katika kipindi cha miezi mitano ijayo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mipango katika kituo hicho Bw. Davud Takfallah, shughuli hizo za Qurani zitajumuisha tamasha za watoto na mabarobaro. Ameliambia shirika la IQNA kuwa sherehe hizo zitafanyika katika miji na mikoa mbali mbali ya Iran na zitajumuisha sana za Qurani, qiraa na hifdhi ya Qurani Tukufu na vile vile Qaswida.
Bw. Takfallah ameongeza kuwa Kituo cha Qurani cha Iran kinatoa masomo ya muda mfupi kuhusu tafsiri ya Qurani kote Iran. Amesema mafunzo hayo yanayotegemea mfumo wa Sheikh Qaraati ni sahali na yanaweza kuhudhuriwa na watu wenye viwango mbali mbali vya elimu.
690378
captcha