Kwa mujibu wa gazeti la Houston Chronicle, Nabil al-Jubeir, msemaji wa Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington amesema kuhusiana na suala hilo kwamba idadi ya mahujaji wa Marekani wanaoelekea Makka kwa ajili ya kuhiji inatazamiwa kuongezeka ikilinganishwa na ya miaka iliyopita. Hii ni katika hali ambayo mwaka uliopita idadi kubwa ya mahujaji wa Marekani walifutilia mbali safari zao za hija kutokana na kuenea maradhi ya mafua ya nguruwe duniani. Maafisa wa Saudi Arabia wamekisia idadi ya mahujai wote watakaohiji mwaka huu kuwa watu milioni 2.5. 693897