IQNA

Mashia wa Saudi Arabia kuomboleza kifo cha Imam Muhammad Baqir (as)

10:48 - November 13, 2010
Habari ID: 2030501
Mashia wa miji ya Kishia nchini Saudi Arabia wamepanga kufanya maombolezo ya kifo cha Imam Muhammad Baqir (as).
Kundi la Sayyid as-Shuhadaa la mjini Dammam limetangaza habari hiyo na kuongeza kwamba maombolezo hayo yamepagwa kufanyika kesho Jumapili katika kituo cha kidini cha Hussein an-Namr al-Musawi.
Abbas al-Mahrus mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini Saudi Arabia atahutubia hadhara ya waombolezaji kuhusiana na shakhsia pamoja na maisha ya imam huyo wa tano wa Ahlul Beit (as).
Maombolezo mengine kama hayo yamepangwa kufanyika leo Jumamosi katika Husseiniyya ya Umm Mueen katika mji wa Qatif. Said al-Maatiq mmoja wa mahatibu na wahubiri wa Kishia wa Sauadi Arabia anatazamiwa kuhutubia waombolezaji katika maombolezo hayo. 693798
captcha