IQNA

Kikao cha Miujiza ya Qur'ani na Sunna kufanyika Istanbul

13:48 - November 13, 2010
Habari ID: 2030871
Uturuki itaandaa kikao cha 10 cha Jumuiya ya Kimataifa ya Miujiza ya Qur'ani na Sunna.
Kwa mujibu wa tovuti ya Moheet, kongamano hilo litafanyika Machi 11-14 mwaka 2011 mjini Istanbul.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Miujiza ya Qur'ani na Sunna Dkt. Abdullah Bin Abdulaziz al Musleh amesema mada kuu ya kikao hicho itakuwa, 'Athari za Miujiza ya Qur'ani katika Fikra ya Mwanadamu'.
Al Musleh ameongeza kuwa washiriki watajadili pia miujiza ya Qur'ani na Sunna katika nyanja mbalimbali za biolojia, falaqi, sayansi za anga za mbali, jiolojia, ubaharia, sayansi za jamii na sheria.
693846
captcha