IQNA

Kongamano la Qur'ani na Masuala ya Kisasa kufanyika Nairobi

14:21 - November 13, 2010
Habari ID: 2030872
Kongamano la kimataifa la 'Qur'ani Tukufu na Masuala ya Kisasa' limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi kwa ushirikiano wa Kitengo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Idara ya Filosofia ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Nairobi, kongamano hilo litawashirikisha wasomi na watafiti ambao watajadili masuala kama vile, 'Qur'ani: Masuala ya Kimaadili kuhusu Sayansi ya Kisasa, Qur'ani na Botania, Qur'ani na Afya, Qur'ani na Embriolojia, Qur'an na Sayansi za Kisasa, Qur'ani na Anga za Mbali, Qur'ani na Uadilifu wa Kiuchumi, Qur'an na Masuala ya Mazingira, Qur'ani na Changamoto Zinazomkabili Mwanadamu Duniani, Qur'ani: Masuala ya Kifilosofia na Kianthropolojia na Qur'ani na Masuala ya Dini Mbalimbali.
Kongamano hilo litafanyika kuanzia Machi 10-12 mwaka 2011 katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya.
Wanaotaka kushiriki katika kongamano hilo wanatakiwa kuwasilisha mukhtasari wa makala zao kufikia Februari 15, 2011.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Idara ya Utamaduni ya Jamburi ya Kiislamu ya Iran, SLP 59595-00200 Nairobi-Kenya
Simu +245 20 2214352 +254 20 318833
Barua pepe: iranlib@yahoo.com

694264
captcha