Kituo cha habari cha "c-el" kimeripoti kuwa masomo hayo ambayo yataendelea kwa kipindi cha wiki kumi yatatolewa kwa shabaha ya kuwaelimisha Waislamu wapya Qur'ani na itikadi za Kiislamu.
Masomo hayo yatatolewa katika viwango vitatu vya awali, kiwango cha kati ya masomo ya juu katika nyanja za kusoma Qur'ani, somo la sheria za Kiislamu, itikadi na maadili ya Kiislamu.
Masomo kama hayo makhsusi kwa wanaume yanatolewa kwa sasa katika Kituo cha Kiislamu cha London.
Kituo hicho pia kimepanga kuitisha kikao cha dua ya Arafa Jumanne tarehe 16 Novemba na sherehe za Idul Haji tarehe 17 Novemba. 694227