Watu wengi katika nchi za kimagharibi kama vile Australia, New Zealand, Uingereza na nchi za Asia kama vile Korea Kusini na Singapore wanavutiwa sana na mfumo wa benki za Kiislamu.
Kwa mujibu wa jarida la Global Islamic Finance Magazine, Richard Thomas mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Gatehouse ya London amesema, ‘hivi sasa tunashuhudia kuongezeka mapendekezo ya kutumia mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu hasa katika taasisi za kiuchumi za nchi zisizo za Kiislamu’. Akizungumza katika Kongamano la Kimataifa la Uhasibu nchini Malaysia, Thomas amesema, ‘ kumeshuhudiwa ustawi katika utumizi wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu miongoni mwa benki na taasisi zingine za kiuchumi kote duniani’.
Katika kongamano hilo, Thomas amewasilisha makala chini ya anuani ya ‘Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu na Uimarishwaji Masoko ya Dunia’. Mtaalamu huyo wa uchumi amesema kiwango cha ustawi wa uchumi wa Kiislamu duniani ni asilimia 7. Ameongeza kuwa ‘Mfumo wa kifedha wa Kiislamu una uwezo wa kustawi kwa kasi zaidi lakini baadhi ya sheria za kodi na uhasibu zinakwamisha ustawi wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu katika nchi mbalimbali za dunia’. 694642