IQNA

Tamasha la sita la Idul Adh'ha kufanyika Qatif, Saudi Arabia

14:48 - November 14, 2010
Habari ID: 2031758
Tamasha la sita la Udul Adh'ha limepangwa kufanyika tarehe 27 hadi 29 katika mji wa Qatif nchini Saudi Arabia.
Tamasha hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Huduma za Kijamii ya al-Jarudiyya. Maonyesho ya sanaa za mikono, ratiba tofauti za kidini na kiutamaduni, michezo ya kuigiza ya kijamii, warsha za mafunzo na mashindano ya kiutamaduni na kisanaa ni miongoni mwa mambo yatakayotekelezwa katika tamasha hilo la siku tatu.
Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Huduma za Kijamii ya al-Jarudiyya itakuwa ikitekeleza ratiba za tamasha hilo kuanzia saa kumi na mbili hadi saa mbili usiku. 694582
captcha