IQNA

Chama cha Die Grünen Ujerumani chataka kuanzishwa masomo ya Kiislamu mashuleni

15:50 - November 14, 2010
Habari ID: 2031909
Chama cha Kijani cha Ujerumani (Die Grünen) kimeitaka serikali ya nchi hiyo kuanza kutoa masomo ya Kiislamu katika shule zote za jimbo la Nordrhein-Westfalen nchini humo.
Kituo cha habari cha dunyabulteni kimeripoti kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kijani cha Ujerumani katika jimbo la Nordrhein-Westfalen Monika Düker ameitaka serikali ya nchi hiyo kuanza kutoa masomo ya Kiislamu katika shule za jimbo hilo katika mwaka wa masomo wa 2011-2012 hususan kwa wanafunzi Waislamu.
Vilevile ameitaka Jumuiya ya Kiislamu ya Ujerumani na mabaraza manne ya Kiislamu nchini humo kubuni mitaala ya masomo ya Kiislamu kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.
Mwanasiasa huyo wa Ujerumani anasema kuwa kwa sasa zaidi ya wanafunzi laki tatu na 20 elfu wa Kiislamu wanajishughulisha na masomo katika jimbo la Nordrhein-Westfalen na kwamba ni Waislamu karibu elfu 11 tu ndio wanaoweza kupata elimu ya maarifa ya Kiislamu. 695367

captcha