IQNA

Sala ya Idul Adh'ha kusaliwa Jumatano katika Chuo Kikuu cha Tehran

12:54 - November 15, 2010
Habari ID: 2032045
Sala ya Idul Adh'ha katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran itasaliwa Jumatano katika Chuo Kikuu cha Tehran.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kamati ya Sala ya Ijumaa ya Tehran, Hujjatul Islam Yadollah Shirmardi, Sala ya Idul Adh'ha mwaka huu itaongozwa na Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khatami.
Amesema sikukuu ya Idul Adh'ha ina umuhimu mkubwa katika umma wa Kiislamu na inapaswa kusherehekewa kwa taadhima.
Kuhusu mipango ya Sala, amesema kutakuwa na maafisa 4000 wa polisi na huduma za dharura za afya katika eneo la Chuo Kikuu cha Tehran.
Waislamu kote duniani watajiunga na mahujaji walio Makka katika kusherehekea Idul Adh'ha.
695325




captcha