Kwa mujibu wa tovuti ya Haj Information, wizara iliyotajwa imetayarisha magari maalumu 124 yanayotumia umeme yatakayowawezesha mahujaji wazee na vilema kurushia mawe mashetani wakiwa juu ya daraja la Jamarat.
Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa mahujaji hao watatumia magari hayo katika msimu wote wa hija bila kutoa malipo yoyote. Kila moja kati ya magari hayo lina uwezo wa kubeba mahujaji 14 kutoka kwenye kambi zao na kuwawezesha kutekeleza amali ya kumrushia mawe shetani na kisha kuwarejesha kwenye kambi hizo.
Huduma hiyo imekaribishwa na mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu. 695378