IQNA

Pazia la al-Kaaba labadilishwa leo

12:32 - November 15, 2010
Habari ID: 2032337
Pazia la al-Kaaba Tukufu limebadilishwa leo Jumatatu tarehe 15 Novemba, ambayo ni siku ya Arafa nchini Saudi Arabia. Pazia hilo limebadilishwa baada ya kuoshwa kwa maji ya marashi kutoka mji wa Kashan nchini Iran katika sherehe maalumu.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia, Muhammad bin Nassir al-Khuzaim, naibu mkuu anayesimamia masuala ya Masjidul Haram amesema kuwa pazia hilo limetengenezwa kutokana na kitambaa cha hariri halisi cha rangi nyeusi.
Makumi kadhaa ya kilo za dhahabu na shaba yametumika katika urembeshaji na itiaji nakshi aya za Qur'ani zilizoandikwa kwenye pazia hilo. Amesema sherehe hiyo maalumu ya kubadilisha pazia la al-Kaaba imeonyeshwa moja kwa moja kwa watazamaji kupitia anwani ifuatayo ya mtandao wa intaneti: www.gph.gov.sa.
Pazia hilo limefumwa kutokana na vitambaa vitano ambapo kila kimoja kinafunika upande mmoja kati ya pande nne za al-Kaaba na kitambaa cha tano kinafunika mlango wa al-Kaaba. Pazia hilo zima lina uzito wa karibu tani mbili. Thamani ya pazia hilo ni riali milioni 20 za Saudi Arabia na limeshonwa katika mojawapo ya karakana za nchi hiyo.
Kitambaa cha pazia hilo hutolewa kila mwaka na moja ya nchi za Kiislamu. Ushonaji na utayarishaji wa pazia hilo kwa kutumia mikono na mashine huchukua karibu miezi minane. 695812
captcha