IQNA

Kongamano la Maqari wa Qur'ani Tehran

12:35 - November 15, 2010
Habari ID: 2032382
Kongamano la Nane la Maqari na Wanaharakati wa Qur'ani linafanyika leo Novemba 15 katika Msikiti wa Jamia wa Imam Sadiq (AS).
Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Qur'ani cha Tehran kwa lengo la kuwaenzi maqari, wataalamu na wanaharakati wa Qur'ani mjini Tehran.
Gholamreza Rabieian, Nasrollah Ghasemi, Ali Soleymani, Majid Davoodi na Shamsi Ahmadi ni kati ya maqari watakaoenziwa katika kongamano hilo.
Kongamano hilo hufanyika kila mwaka katika Msikiti wa Jamia wa Imam Sadeq (AS) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya waumini wanaoihudumia Qur'ani Tukufu.
695497
captcha