Mohsen Pakayin ameyasema hayo mjini Tehran Jumatatu 15 Novemba katika sherehe za kuanzishwa vitengo vya lugha za Myanmar na Kazakh katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA.
Ameongeza kuwa ni fakhari kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa shirika la kwanza la habari za Qur'ani duniani liko katika nchi ya Kishia.
Amesema katika dunia ya leo, kuarifisha Qur'ani kwa walimwengu na kueneza mafundisho yake ni masuala muhimu mno ili kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na hujuma ya kipropaganda ya maadui.
Kwa kuongezwa lugha hizo mbili, idadi ya lugha katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa imefika 31.
696172