Kwa mujibu wa mkuu wa Shirika la Shughuli za Qur'ani za Wanachuo wa Iran Bw. Issa Alizadeh, mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Harakati ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Khorasan Razavi na taasisi kadhaa za Qur'ani.
Ameongeza kuwa, 'Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka zaidi ya nchi 40 watashindana katika viwango vya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na qiraa katika ukumbi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.
Mashindano hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza Aprili 2006 kwa ushirikiano na Manispaa ya Mji wa Isfahan na duru ya pili ilifanyika mwaka 2008 katika Mnara wa Milad mjini Tehran kwa ushirikiano na Manispaa ya Mji wa Tehran.
698037