Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za ufunguzi wa olimpiadi hiyo zimefanyika Jumapili Novemba 21 katika Idara ya Ustawi wa Kiislamu mjini Qum na kuhudhuriwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW Ayatullah Reza A’rafi na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran anayeshughulikia masuala ya Qur'ani Hujjatul Islam Hamid Muhammadi.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi msimamizi wa masuala ya elimu na utamaduni katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW Hujjatul Islam Salehi amesema, ‘zaidi ya wanachuo 9000 wa chuo hicho na familia zao walishiriki katika awamu ya kwanza ya olimpiadi hiyo. Ameongeza kuwa wanachuo 120 wa kike na kiume wamefuzu kuingia fainali ya olimpiadi hiyo ambayo itamalizika Novemba 24.
Akizungumza katika sherehe hizo Ayatullah A’rafi amewashukuru waandaaji na washiriki wa olimpiadi hiyo. Aidha amebainisha sera na programu za Qur'ani za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW.
698137