IQNA

Msikiti wa Imam Ali (as) waandaa sherehe ya Idi Ghadir Khum

14:56 - November 21, 2010
Habari ID: 2034981
Msikiti wa Imam Ali (as) katika mji wa Istanbul nchini Uturuki unaandaa leo Jumapili sherehe maalumu ya kusherehekea Idi Ghadir Khum.
Kwa mujibu wa tovuti ya Msikiti wa Zainabiyya wa mjini Istanbul, sherehe hiyo itaanza mara tu baada ya kusimamishwa swala za Adhuhuri na Alasiri. Mashia na wapenzi wa Maimamu watoharifu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) wanatazamiwa kushiriki kwa wingi katika sherehe hiyo, itakayofanyika katika msikiti uliotajwa katika mtaa wa Bağcılar.
Jana pia Mashia wa Uturuki katika mji wa Igdir walijumuika katika sherehe nyingine kama hiyo. Sherehe nyingine kama hiyo imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa Novemba 26 na kuhudhuriwa pia Wanazuoni wa Ahlul Bait (as) katika mji wa Igdir. 698652
captcha