Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yametembelewa na Ayatullah A’rafi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayeshughulikia masuala ya Qur'ani Hujjatul Islam Hamid Muhammadi. Maonyesho hayo yanafanyika pembizoni mwa fainali ya Olimpiadi ya Qurani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW.
Msimamizi wa maonyesho hayo, Mehdi Sabbaghi amesema yataendelea hadi Novemba 24.
Maonyesho hayo yana vibanda 26 kutoka vitengo tofauti vya chuo hicho kikuu na vile vile vibanda vinne vya taasisi kadhaa zinazoonyesha mafanikio yao katika masuala ya Qur'ani na Hadithi.
Maonyesho hayo yanayofanyika katika Kituo cha Maendeleo ya Kiislamu cha Qum yanafunguliwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku.
697800