Ja’afar Ibrahim kutoka Sudan ndiye aliyekuwa mshiriki wa mwisho kujibu maswali ya jopo la majaji. Alishiriki katika kitengo cha kuhifadhi Juzuu 15 za Qur'ani Tukufu.
Baada ya kumalizika mashindano ya wanaume, qari wa kimataifa Ustadh Saeedian alisoma aya za Qur'ani Tukufu kwa sauti iliyowavutia hadhirina. Aidha kulikuwa na qasida kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Hadi AS.
Mashindano ya wanawake yanatazamiwa kumalizika leo Novemba 22 katika ukumbi wa Idara ya Ustawi wa Kiislamu mjini Qum.
699609