Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo linahudhuriwa na washiriki 1,200 kutoka zaidi ya nchi 50 duniani.
Kongamano hilo la siku tatu linafanyika kwa hisani ya Mwanamfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa Waziri Mkuu wa Bahrain na udhamini wa Benki Kuu ya Bahrain.
Maudhui kuu ya kongamano la mwaka huu ni , ‘Kuanzisha kielelezo kipya cha ustawi, Benki za Kiislamu na upeo mpya wa kifedha duniani’.
Washiriki wa kongamano hilo ni wataalamu katika uga wa mfumo wa fedha wa Kiislamu na watajadili changamoto zinazoukabili mfumo wa kifedha wa Kiislamu duniani.
Pembizoni mwa kongamano hilo kutakuwa na Maonyesho ya Benki za Kiislamu Duniani ambapo mashirika 60 yataonyesha ubunifu wao katika mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
699542