IQNA

Wanigeria wana hamu kubwa ya kuujua Ushia

16:38 - November 22, 2010
Habari ID: 2035988
Wananchi wa Nigeria wana hamu kubwa ya kuujua Ushia na mafundisho ya Ahlul Beit (as).
Hayo yamesemwa na Shuaib Muhammad, mwanafunzi wa masomo ya kidini wa Nigeria ambaye anasimamia kibanda cha nchi za Kiafrika katika maonyesho ya Qur'ani na hadithi yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya al-Mustafa (saw) katika mji mtakatifu wa Qum. Akizungumza na shirika la habari la IQNA mwanafunzi huyo amesisitiza kwamba licha ya Mawahabi na Wakristo kutumia fedha nyingi kwa lengo la kueneza fikra zao nchini Nigeria lakini kuna mazingira mazuri ya kuenea mafundisho ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) nchini humo. Ameashiria juhudi kubwa za kitablighi za kuanzisha vituo vya Qur'ani na kidini zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa ya al-Mustafa nchini Nigeria na kuongeza kuwa jumuiya hiyo imechangia pakubwa katika kuwafanya Wanigeria wengi kuwa Mashia.
Maonyesho hayo ya Qur'ani na hadithi yaliyoanza siku ya Jumamosi Novemba 20 yataendelea hadi siku ya Jumatano Novemba 24. 699192
captcha