IQNA

Kambi ya watoto ya Mafunzo ya Kiislamu Malaysia

12:27 - November 23, 2010
Habari ID: 2036213
Msikiti wa Kitaifa wa mji wa Kuala Lumpur nchini Malaysia umeandaa kambi ya mafunzo ya kidni kwa ajili ya watoto walio na umri wa miaka 9-11 kwa muda wa siku tatu kuanzia Disemba 10.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kambi hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa Kitengo cha Ustawi wa Kiislamu cha Malaysia JAKIM na inakusudia kulea kizazi cha wananchi watiifu walio tayari kukabiliana na changamoto za maisha na kufuzu katika maisha ya dunia na akhera.
Taarifa iliyotolewa imesema washiriki wa kambi hiyo watapewa mafunzo na wanachuo wa vyuo vikuu vya Malaysia.
Watoto wa Malaysia wana muda wa kufikia tarehe 3 Disemba kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki katika kambi hiyo.
699816

captcha