IQNA

Maeneo mataaktifu kusafishwa baada ya Hija

12:24 - November 23, 2010
Habari ID: 2036215
Zaidi ya wafanyakazi wa elfu kumi na tatu wameanza zoezi la kusafisha maeneo matakatifu ya mji wa Makka al Mukarramah baada ya kumalizika Ibada ya Hija.
Meya wa Makkah Dr. Osama bin Fadhl al Bar amesema ndege za Wizara ya Kilimo zitatumika kunyinyiza dawa za kusafisha maeneo matakatifu na kuangamiza vijidudu maradhi. Aidha wafanyakazi elfu kumi na tatu wakiwa na mashine elfu moja mia mbili za usafi wameanza zoezi za kuusafisha mji mtakatifu wa Makka.
Zoezi hilo la usafishaji litajumuisha maeneo matakatifu ya mji wa Makkah kama vile Mina, Arafat, Muzdalifa na maeneo ya karibu.
699959


captcha