IQNA

Chuo cha Kiislamu cha California kinaendelea kustawi

10:21 - November 24, 2010
Habari ID: 2037093
Chuo cha Zaytuna ambacho ni chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu nchini Marekani kilichofunguliwa hivi karibuni kwa shabaha ya kuendeleza dini ya Kiislamu na kuzima njama na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo, kinaendelea kustawi na kupanua zaidi shughuli zake.
Darasa la kwanza katika chuo hicho lilianza likiwa na wanafunzi 15 katika eneo la kukodishwa ndani ya Chuo Kikuu cha California. Sasa Chuo cha Zaytuna kimekusudia kuwa chuo kikubwa na chenye itibari kama vyuo vikuu mashuhuri vya Marekani.
Maafisa wa chuo hicho wanaamini kwamba ubaguzi unaowasumbua Waislamu ulizikumba pia jamii nyingine za kidini katika karne za 19 na 20 ambazo sasa zimekubalika katika jamii ya Marekani.
Chuo cha Kiislamu cha Zaytuna kinatoa elimu ya fasihi ya Kiislamu, sheria na teolojia na historia na wafuasi wa dini zote wanaruhusiwa kuhudhuria masomo hayo.
Kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew, karibu Waislamu milioni sita wanaishi nchini Marekani. Vilevile kuna zaidi ya misikiti 2000 na shule 500 za Kiislamu katika maeneo mbalimbali ya Marekani. 700659


captcha