IQNA

Olimpiadi ya 16 ya Qurani na Hadithi yakamilika

12:36 - November 26, 2010
Habari ID: 2037311
Olimpiadi ya 16 ya Qurani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Moustafa SAW maalumu kwa wanachuo wasio Wairani imemalizika mjini Qum Jumatano 24 Novemba katika sherehe zilizohudhuriwa na Dr. Sayyed Mohammad Husseini Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hizo zilianza kwa kusomwa Qurani Tukufu na Muadh Mustafa kutoka Thailand ambaye pia alipata nafasi ya kwanza katika mashindano ya qiraa. Sherehe hizo zimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Idara ya Utangazaji Uislamu.
Akizungmza katika halfa hiyo mkuu wa masuala ya utamaduni na ulezi katika ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW amesema kuwa Olimpiadi ya wanachuo wa kidini wasio Wairani imewavutia wengi na ilikuwa na ubunifu katika sekta mbali mbali. Amesema kwa ujumla Olimpiadi hiyo ilikuwa na washiriki elfu tisa kutoka mataifa 87 na kwamba mashindano yalifanyika katika nchi 34 duniani katika vitengo 56 ambapo washiriki 120 walifika katika fainali. Akizungmza katika hafla hiyo, Dr. Sayyed Mohammad Husseini Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ameashiria kufanyika Olimpiadi hiyo katika kipindi hiki cha sikukuu ya Ghadir Khuma na kusema: “Idi ya Ghadi ni idi kubwa zaidi ya Idul Fitr na Idul Adha na hili linatokana kuwa Qurani Tukufu imeashiria mara kadhaa tukio hili (la Ghadi Khum).”
Ameongeza kuwa siku ya Ghadir ni siku ya watu kujitakasa batini na dhahiri na kuongeza kuwa waumini wanapaswa kuwa na furaha katika siku hii.
Fainali ya Olimpiadi ya 16 ya Qurani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Moustafa SAW ilikuwa na washiriki wa 120 wanaume na wanawake na ilianza tarehe 20 Novemba.
701304


captcha