Hujjatul Islam Walmuslimin Sadruddin al Qubanchi aliyasema hayo katika hotuba za swala ya Ijumaa ya jana katika Husainiya ya al Fatimiyya mjini Najaf na kuongeza kuwa sikukuu na tukio la Ghadir Khum si tukio la zama makhsusi la kihistoria bali ni wito uliotolewa kwa ajili ya wanadamu na Waislamu wa zama zote.
Vilevile amezungumzia mnasaba wa siku ya kimataifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na akasema kuwa mafundisho ya dini ya Kiislamu yanasisitiza juu ya udharura wa kukabiliana na ukatili kama huo na kwamba Mtume Mtukufu (saw) alikuwa akisema: “Mbora wenu ni yule anayekuwa mtu bora kwa ahli yake.” 701878