IQNA

Iran yaanzisha vituo 110 vya Qur'ani duniani

8:35 - November 28, 2010
Habari ID: 2038460
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW cha Qum nchini Iran kimeanzisha vituo 110 vya Qur'ani –Dar-ul-Quran- katika zaidi ya nchi 50 duniani.
Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha utamaduni na elimu cha chuo hicho kikuu Bw. Mohammad Reza Saleh. Amesema vituo 40 vipya vya Qur'ani vimeanzishwa barani Asia na Ulaya.
Saleh amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, ‘Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW kinalenga kusambaza mafundisho ya Qur'ani na Ahul Bayt AS pamoja na maarifa ya Kiislamu kupitia matawi yake duniani’.
Amesisitiza kuwa nguzo za Jamhuri ya Kiislamu zimesimama kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani. Ameongeza kuwa, ‘mwanzilishi wa itikadi hii kama kiongozi shupavu aliongoza harakati ya Kiislamu kwa kutegemea mafundisho ya Qur'ani Tukufu.’.
Amesema kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW kinajitahidi kuhakikisha mtazamo huo unatambulika kote duniani.
701715
captcha