Mji mkuu wa Ugiriki hadi sasa hauna hata msikiti mmoja kwa ajili ya wafuasi wa dini ya Kiislamu licha ya kuwepo idadi kubwa ya Waislamu na wahajiri wengi katika mji huo. Suala hili limewalazimisha Waislamu wa mji huo kutekeleza ibada zao katika magofu na majengo ya zamani ya mji huo.
Kwa kuzingatia hali hiyo, Dhuha Hadid amesema kuwa yuko tayari kuchora ramani ya msikiti wa kwanza kabisa wa mji wa Athens. Msanii huyo mkubwa wa Uingereza amepata umashuhuri mkubwa katika sanaa hiyo na athari yake ya hivi karibuni ni jengo la sanaa za kisasa la jiji la Roma nchini Italia.
Asilimia 90 ya wananchi wa Ugiriki ni Wakristo wa Kanisa la Orthodox
ambalo ni sehemu ya serikali ya nchi hiyo. 702025