IQNA

Uungaji mkono wa Isesco kwa mipango ya kiutamaduni ya Quds Tukufu

16:03 - November 28, 2010
Habari ID: 2038997
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu Isesco na Jumuiya ya Kimataifa ya Wito wa Kiislamu zitasaidia kifedha utekelezwaji wa mipango ya kiutamaduni ya mji mtakatifu wa Quds.
Kwa mujibu wa tovuti ya Isesco, shirika hilo na jumuiya iliyotajwa ya wito wa Kiislamu zitashirikiana katika kuchangia kifedha mipango hiyo pamoja na ya kimalezi katika mji wa Quds. Kuhifadhiwa baadhi ya nuskha zilizoandikwa kwa mkono katika maktaba za Quds, ukarabati wa baadhi ya athari za kale za Kiislamu na utekelezwaji wa mipango ya masomo kwa watu walio na mahitaji maalumu ni baadhi ya mambo yatakayosimamiwa kifedha na jumuia mbili hizo za Kiislamu katika mji mtakatifu wa Quds. Utekelezaji wa mipango maalumu ya Wiki ya Quds mjini Cairo, msaada kwa vituo na taasisi za kiutamaduni za Palestina na mipango ya vituo vya habari na demokrasia vya Palestina ni mipango mingine itakayopata ufadhili wa kifedha wa taasisi mbili hizo za Kiislamu. 702311
captcha