Kwa mujibu wa ic-el semina hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa kituo hicho cha Kiislamu, Jumuiya ya Kiislamu ya Ahlul Beit (as) na Taasisi ya Bani Hashim ya London. Hujjatul Islam wal Muslimeen Muizzi, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha London atazungumzia tukio la kihistoria la Ghadir Khum. Wengine waliopangiwa kuzungumza katika kituo hicho ni pamoja na Ayub Rashid Mbegu atakayezungumzia suala la umuhimu wa uimamu kwa ajili ya umma wa Kiislamu na tofauti yake na utume na vilevile Muhammad Zakariya atakayezungumzia mafunzo ya Ghadir. Kituo hicho cha Kiislamu cha London pia siku ya Alkhamisi Novemba 25 kiliandaa sherehe maalumu ya kuadhimisha siku ya Ghadir Khum kwa ajili ya kuhuisha tukio la kihistoria la Ghadir Khum la kukabidhiwa Imam Ali (as) uongozi wa umma wa Kiislamu na Mtume Mtukufu (saw). 702107