Fainali ya mashindano ya 24 ya Qur'ani ya wafanyakazi wa kitengo cha anga za juu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, inatazamiwa kufanyika Januari 3-5 mwaka 2010.
Kwa mujibu wa Kanali Asadollah Samari Mkurugenzi wa Chuo cha Qur'ani (Darul Qur'an) cha IRGC, mashindano hayo yatafanyika katikaUkumbi wa Utamaduni wa Al Ghadri katika Makao Makuu ya Makamanda wa IRGC mjini Tehran.
Mashindano hayo yalianza kwa mchujo na yalijumuisha maafisa wa IRGC na vile vile wale wanaofanya huduma ya kitaifa ya jeshi. Imearifiwa kuwa mashindano ya mchujo ya wanawake yalifanyika Oktoba 27-28 ambapo 40 walifuzu kushiriki katika awamu itakayofuata.
Washiriki wanashindana katika vitengo vya hifdhi, qiraa na ufahamu wa Qur'ani Tukufu.
702838