IQNA

Kamati ya masuala ya kibinadamu ya OIC yaenda Gaza

17:51 - November 29, 2010
Habari ID: 2039762
Kamati inayoshughulikia masuala ya kibinadamu ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imeelekea katika Ukanda wa Gaza kwa madhumuni ya kwenda kuratibu mipango ya ufikishaji misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa ukanda huo unaozingirwa na utawala ghasibu wa Israel.
Kamati hiyo inayoongozwa na Fuad Maznai, mkuu wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya kibinadamu ya OIC inajumuisha madaktari na wawakilishi wa nchi tofauti za Kiislamu wanachama wa OIC. Kamati hiyo inalenga kuratibu njia za kushirikiana zaidi OIC na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu kwa madhumuni ya kuwahudumia wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Timu ya madaktari itatafuta njia za kuwahudumia kitiba wakazi wa Ukanda wa Gaza na kutoa mafunzo ya tiba kwa wafanyakazi wa sekta ya tiba na afya ya ukanda huo.
Kamati hiyo ya OIC itakutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Gaza pamoja na mashirika ya kimataifa ya utoaji misaada ya kibinadamu kwa shabaha ya kuchunguza mahitaji ya dharura zaidi yanayohitajiwa na wakazi wa ukanda huo. 702794
captcha