Akijibu maswali ya mwandishi wa IQNA katika kikao na waandishi habari wa ndani na nje ya nchi mjini Tehran, amesema katika duru ya tatu ya kutembelea mikoa yote ya Iran, moja ya masuala ambayo yanayopewa umuhimu ni shughuli za Qur'ani.
Mwanzoni mwa kikao chake na waandishi habari, Rais Ahmadinejad amesema mfumo wa kibepari duniani unakaribia kusambaratika na kwambo umegonga mwamba katika masuala mbalimbali duniani. Amesema ulimwengu unahitaji fikra, njia na mfumo mpya. Ameongeza kuwa: "Itikadi yetu ni kuwa, watenda mema duniani wanapaswa kuungana na kuanzisha mfumo mpya ambao utaheshimu haki za mataifa na kuzingatia heshima ya mwanadamu, mfumo ambao utayashirikisha mataifa yote.
Akimjibu mwandishi wa kanali ya Press TV aliyeuliza swali kuhusu nyaraka zilizosambazwa na tovuti ya WikiLeaks, Rais Ahmadinejad amesema kuwa nyaraka hizo hazina thamani yoyote ya kisheria.
Amesema kuwa nyaraka hizo hazikufichuliwa bali zinatolewa kwa mpangilio maalumu kwa malengo ya kisiasa. Amesema kuwa nyaraka hizo zinashabihiana zaidi na vita vya kipropaganda na kisaikolojia. 704017