IQNA

Historia ya Uislamu kuchunguzwa Brussels

7:48 - November 30, 2010
Habari ID: 2039900
Vikao vya Uchunguzi wa Historia ya Uislamu vitaanza wiki ijayo katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels kwa hima ya Msikiti wa al Tauba.
Kituo cha habari cha Islamic-events kimeripoti kuwa vikao hivyo vitafanyika siku za Jumatano na Alkhamisi kila wiki vikihudhuriwa na Sheikh Sabahi, mhadhiri wa taaluma za Kiislamu ambaye pia ni miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini Ubelgiji.
Mada zitakazojadiliwa katika vikao hivyo ni pamoja na kukamilika Utume katika mtazamo wa Kiislamu, vita vya Waislamu na washirikina, kuanza utume wa Nabii Muhammad (saw), safari ya miraji, kubadilishwa kibla cha Waislamu na maisha ya Nabii Muhammad (saw) na mwenendo wake na wafuasi wa dini nyingine.
Vilevile masomo ya lugha ya Kiarabu na taaluma za Kiislamu yatatolewa katika msikiti wa al Tauba. 703642
captcha