IQNA

Mwakilishi wa Libya katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Mash'had:

Mashindano ya Qur'ani ya wanachuo yanachangia katika kuimarisha thamani za Kiislamu

12:47 - December 01, 2010
Habari ID: 2040702
Kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika kiwango cha wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu kunachangia mno katika kueneza na kuimarisha zaidi utamaduni na thamani za Kiislamu na kustawisha zaidi uhusiano kati ya nchi za Waislamu.
Hayo yamesemwa na hafidhi wa Qur'ani na mwakilishi wa Libya katika mashindano ya tatu ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanachuo wa Kiislamu Badruddin Abdul Hakiim. Amesema kuwa kufanyika mashindano hayo katika mji mtakatifu wa Mash'had kunawapa washiriki fursa ya kutembelea maeneo matakatifu ya mji huo.
Badruddin al Hakiim ameongeza kuwa miongoni mwa sifa za karii hodari wa Qur'ani ni uwezo wa kutamka vyema na kwa njia sahihi herufi za kitabu hicho. Amesema kuwa hadi sasa ameshiriki katika mashindano mbalimbali ya Qur'ani nchini Libya na kupata nafasi za kwanza, pili na tatu. Amesema kuwa alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu mwaka 1997 na kwamba kuhifadhi Qur'ani kumekuwa na taathira kubwa katika nafsi yake. 704405

captcha